• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatoa wito kutoa huduma za kimsingi za afya wakati wa kukabiliana na janga la virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-31 09:03:37

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema kila nchi inapaswa kuendelea kutoa huduma za msingi za kiafya wakati wa kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

    Bw. Tedros amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari, na kuongeza kuwa WHO imetoa mwongozo wa kusaidia nchi kudumisha uwiano kati ya kudhibiti janga hilo na kutoa huduma za kimsingi za afya, ili kupanga upya na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za hali ya juu za afya, ikiwemo chanjo za kawaida, ujauzito na kujifungua, matibabu ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, magonjwa ya akili na huduma za damu.

    Aidha Bw. Tedros amesema WHO imejadiliana na mawaziri wa biashara wa kundi la G20 kuhusu jinsi ya kutatua tatizo la upungufu wa vifaa vya kujikinga na vifaa vingine vya matibabu, na kutoa wito kwa serikali kufanya kazi na kampuni binafsi kuongeza uzalishaji, kuhakikisha mgawanyo wenye usawa wa bidhaa muhimu za matibabu kutokana na mahitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako