• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya ushirikiano wa dunia katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona yaharakishwa

    (GMT+08:00) 2020-03-31 10:23:16
    Katika kipindi muhimu cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani, Mkutano maalumu wa viongozi wa kundi la G20 wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona uliofanyika tarehe 26 Machi, umeonesha ishara chanya ya nchi mbalimbali kushirikiana kupambana na ugonjwa huo. Hivi karibuni China na nchi mbalimbali duniani zimeharakisha mchakato wa ushirikiano katika utafiti wa chanjo ya virusi na mambo ya matibabu, na kutoa misaada ya vitu vya matibabu kwa nchi mbalimbali, na hatua ya ushirikiano wa dunia katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona inaharakishwa.

    Ili kukabiliana na hali mbaya ya maambukizi ya virusi vya Corona, kazi kuu ni utafiti na utengeneza wa chanjo. Usiku wa tarehe 26, rais Xi Jinping wa China alitoa wito kwenye mkutano maalumu wa viongozi wa kundi la G20 wa kupambana na ugonjwa huo, kuwa nchi zote zinatakiwa kushirikiana kuharakisha hatua ya utafiti wa sayansi wa dawa, chanjo na upimaji, ili kupata matokeo yatakayonufaisha binadamu wote haraka iwezekanavyo.

    Naibu waziri wa sayansi na teknolojia ya China Bw. Xu Nanping

    Wakati huo huo, China imekuwa ikitoa misaada ya vitu vya matibabu kwa nchi mbalimbali duniani kadiri iwezavyo.

    Tangu maambukizi ya virusi hivyo yalipoenea barani Ulaya, China imepeleka timu nyingi za wataalamu wa matibabu zikiwa na vitu vingi vya matibabu katika nchi zilizoathiriwa vibaya zaidi ikiwemo Italia.

    Timu ya mkoa wa Shandong wa China inayojiunga na kikundi cha pamoja cha kazi cha Uingereza yaelekea Uingereza

    Barani Asia, mbali na kutoa misaada ya matibabu kwa Iran na Iraq, hivi karibuni timu za wataalamu wa matibabu wa China zikichukua vitu vya matibabu zimefika Pakistan, Combodia, na Laos.

    Barani Afrika, tarehe 22 Machi, michango iliyotolewa na mifuko ya Jack Ma na Alibaba kwa nchi mbalimbali za Afrika ikiwa na mask, nguo za kujilinda na vitendanishi imesafirishwa kwenda Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. Hivi sasa vitu hivyo vinasambazwa katika nchi 54 barani Afrika.

    Maambukizi ya virusi hayajali mipaka ya nchi, binadamu wote wanakabiliana na hatma ya pamoja. Kama rais Xi Jinping alivyosema kwenye mkutano maalumu wa viongozi wa kundi la G20 wa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, ili kukabiliana na ugonjwa huo, jumuiya ya kimataifa inachotakiwa kufanya ni kuimarisha imani, kushirikiana na kukabiliana kwa mshikamano. Endapo nchi mbalimbali zitasaidiana mbele ya matatizo, hakika zitashinda mapambano dhidi ya ugonjwa huo, na kupata mustakabali mzuri wa maendeleo ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako