• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa wito wa kutoa dola trilioni 2.5 kuunga mkono nchi zinazoendelea

    (GMT+08:00) 2020-03-31 10:26:16

    Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutoa dola za kimarekani trilioni 2.5 kwa nchi zinazoendelea, ambazo theluthi mbili ya watu wake watakabiliwa na hasara kubwa ya kiuchumi kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona unaoenea kote duniani.

    Ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTD inaonesha kuwa tangu janga la virusi vya Corona lilipoanza, nchi zinazoendelea zimekumbwa na hasara kubwa kutokana na kuondoka kwa mitaji, kushuka kwa thamani ya sarafu na kupungua kwa mapato yanayotokana na uuzaji bidhaa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako