• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya Kimataifa ya Dubai yanatarajiwa kuahirishwa kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-31 17:00:12

    Shirika la Habari la Reuters limesema, Maonyesho ya Kimataifa ya Dubai ya mwaka 2020 huenda yataahirishwa kutokana na kuenea kwa virusi vya Corona kote duniani.

    Nchi wanachama wa Shirikisho la Maonyesho ya Kimataifa zitaitisha mkutano kutoa uamuzi wa mwisho juu ya kuahirisha kufanya maonyehso hayo au la. Kamati ya Maonyesho ya Kimataifa ya Dubai imeeleza kufuatilia kuenea kwa virusi vya Corona duniani, na inapendekeza kuahirisha kufanya maonyesho hayo kwa miezi kadhaa au mwaka mzima.

    Maonyesho hayo yalipangwa kufanyika kuanzia tarehe 20 mwezi Oktoba mwaka huu hadi tarehe 10 mwezi Aprili mwakani, ambayo ni mara ya kwanza kufanyika katika Mashariki ya Kati, na yangewavutia mamilioni ya watalii kutoka nchi zaidi ya 190. Katika miaka ya karibuni, serikali ya Dubai imetumia mabilioni ya dola za kimarekani kujenga na kuboresha miundombinu kwa ajili ya maonyehso hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako