• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Alama za uzalishaji ya China yaonyesha kuimarika katika mwezi Machi wakati mlipuko wa COVID-19 ukipungua

    (GMT+08:00) 2020-03-31 17:47:33

    Alama ya Usimamizi wa Manunuzi nchini China (PMI) katika sekta ya uzalishaji imeonyesha kuongezeka kwa alama 52 kwa mezi Machi kutoka 35.7 ya mwezi Februari.

    Mtakwimu mwandamizi wa Mamlaka ya Takwimu ya China (NBS) Zhao Qinghe amesema, kufufuka huko kumekuja wakati juhudi kubwa za China katika kuratibu udhibiti wa mlipuko wa COVID-19 na maendeleo ya uchumi na jamii zikionyesha mafanikio.

    Amesema asilimia 96.6 ya viwanda vikubwa na vya ukubwa wa kati vimeanza uzalishaji, ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.7 kutoka mwezi mmoja uliopita.

    Wakati huohuo, Idara ya Taifa ya Ushuru nchini China imesema, kiasi cha kodi na ushuru uliokatwa kimefikia dola za kimarekani bilioni 56.8 katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka. Ofisa wa Idara hiyo Wang Daoshu amesema, kiasi cha punguzo la kodi na ushuru kinatarajiwa kuopngezeka zaidi wakati sera mpya zinazolenga kuondoa mzigo kwa viwanda vidogo na biashara binafsi zitakapoanza kutekelezwa kuanzia mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako