• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yasisitiza kuzingatia udhibiti wa watu wenye maambukizi lakini wasio na dalili

    (GMT+08:00) 2020-03-31 17:52:08

    Mkutano wa timu ya uongozi wa kazi za kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 nchini China umetaka mikoa yote kuzingatia udhibiti wa watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona lakini wasioonyesha dalili na kufanya upimaji wa RNA kwa watu wote wanaoingia China.

    Mikoa mbalimbali ya China imeongeza nguvu ya kuwakagua watu walio karibu na wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona na watu wanaoambukizwa wasio na dalili, kuzingatia kukagua maeneo muhimu na watu wenye hatari zaidi ya kuambukiza. Watu wenye maambukizi lakini wasio na dalili wakigunduliwa, ni lazima wawekwe karantini, kutoa habari wazi na kutafuta chanzo cha maambukizi kwa haraka ili kuwaweka watu walio karibu nao karantini pia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako