• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatoa wito wa kushirikiana na kuchukua hatua za pamoja katika kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-31 17:53:09

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Ghebreyesus jana amesema nchi zote duniani zinaanza kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Amesema nchi za G20 zimeahidi kufanya juhudi za kuipatia dunia vifaa vya matibabu kwa haki na usawa, hali ambayo inaonyesha kuwa nchi zote duniani zinaanza kushikamana.

    Tedros amesema WHO inatoa wito kwa nchi zote zishirikiane na makampuni mbalimbali katika kuongeza uzalishaji, na kuhakikisha usafirishaji wa vifaa vya matibabu bila ya kizuizi, na kuvigawa kwa usawa kulingana na mahitaji.

    Wakati huohuo, mkurugenzi mtendaji wa miradi ya dharura ya WHO Bw. Michael Ryan amesema, ingawa nchi nyingi duniani zimechukua hatua ya kufunga mipaka yao, lakini bado hatua nyingi zaidi za kiafya zinapaswa kuchukuliwa, ili kutafuta wagonjwa wote wekiwemo wale wenye hali nzuri na kuwaweka karantini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako