• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa watoa wito wa kuzipatia nchi zinazoendelea msaada wa dola trilioni 2.5 za kimarekani

    (GMT+08:00) 2020-03-31 17:53:36

    Theluthi mbili ya watu kutoka nchi zinazoendelea isipokuwa China wanakumbwa na hasara kubwa ya kifedha kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, na kuufanya Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kuzipatia nchi hizo msaada wa dola trilioni 2.5 za kimarekani.

    Ripoti iliyotolewa na Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mambo ya biashara na maendeleo imeonyesha kuwa, tangu virusi vya Corona vianze kuenea kote duniani, nchi zinazoendelea zimepata hasara kubwa, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mitaji, kushuka kwa thamani ya sarafu, na kupungua kwa mapato yanayotokana na bidhaa zinazouzwa kwa nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako