• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Serikali ya Tanzania yaionya TFF, kisa Ligi Kuu Bara

    (GMT+08:00) 2020-03-31 18:10:30

    Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutangaza ligi zitachezwa bila mashabiki kutokana na tishio la virusi vya Corona, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo, amelitaka shirikisho hilo kutokurupuka na badala yake kufuata maagizo yatakayotolewa na mamlaka husika. Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, alitangaza kusitisha shughuli zote zinazoleta mkusanyiko ikiwamo michezo kwa siku 30 kuanzia Machi 18, mwaka huu, ili kupunguza ongezeko la janga la Corona nchini humo. Singo alisema wizara ilisikia kile kilichozungumzwa na TFF, lakini walifanya haraka kutoa uamuzi kabla ya kujua kipi kitakachotangazwa na serikali baada ya siku 30 kumalizika. Amesema baada ya muda huo kumalizika, wizara husika itakuja na taarifa itakayotoa mwongozo kulingana na hali ya ugonjwa wa Corona itakavyokuwa kipindi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako