• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RUGBY: KRU yafanya mazungumzo na wachezaji wa timu ya taifa

    (GMT+08:00) 2020-03-31 18:10:49

    Shirikisho la Mchezo wa Rugby nchini Kenya (KRU) limethibitisha kuwa mazungumzo yanaendelea kati ya Shirikisho hilo na wachezaji wa timu ya taifa kuhusu mikataba yao katika wakati huu mgumu wa kiuchumi kutojana na maambukizi ya virusi vya Corona. Kutokana na kuwa malipo ya mshahara wao wa mwezi April yanakaribia, wasiwasi umeibuka kama kuahirishwa kwa mashindano na mazoezi kwa lengo la kupunguza maambukizi ya virusi hivyo kunaweza kuathiri vibaya mishahara ya wachezaji hao. Ili kukabiliana na hali hiyo, Shirikisho hilo lilikutana na meneja wa timu ya Kenya Sevens, Eric Ogweno, ambaye aliwafahamisha wachezaji na maofisa wengine wa timu kuhusu suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako