• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona duniani yafikia karibu laki 8

    (GMT+08:00) 2020-03-31 20:14:23

    Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonesha kuwa, hadi kufikia saa moja asubuhi kwa saa za Marekani ya mashariki, watu 800,049 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona duniani, kati yao watu 38,714 wamefariki.

    Takwimu pia zinaonyesha kuwa, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imezidi laki 1.6, na idadi ya watu waliofariki imefikia 2,953.

    Wakati huohuo, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Italia imefikia 101,739 hadi jana jioni, ambayo iliongezeka kwa 4,050, na idadi ya watu waliofariki imefikia 11,591.

    Nchini Uingereza, hadi kufikia saa 3 usiku jana, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona ilifikia 22,141, ambayo imeongezeka kwa 2,619 kwa siku moja.

    Hadi kufikia tarehe 30, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Ufaransa imefikia 44,550 ambao imeongezeka kwa 4,376 ndani ya siku moja, idadi ya watu waliofariki iliongzeka kwa watu 418 ndani ya saa 24 zilizopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako