• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WTO na mashirika ya UM wataka kuhakikisha usalama wa chakula duniani

    (GMT+08:00) 2020-04-01 09:25:08

    Shirika la biashara duniani WTO, Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO na Shirika la Afya duniani WHO jana yametoa taarifa ya pamoja kuzitaka pande mbalimbali kuhakikisha mzunguko huria wa chakula, ili kuhakikisha usalama wa chakula duniani wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Taarifa hiyo ilitolewa na mkurugenzi mkuu wa WTO Roberto Azevêdo, mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu, na mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

    Taarifa hiyo inasema usalama wa chakula na maisha ya mamilioni ya watu kote duniani vinategemea biashara ya kimataifa. Nchi mbalimbali zinapochukua hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, ni lazima zichukue hatua za kupunguza athari za mapambano dhidi ya virusi vya Corona kwa utoaji wa vyakula, na athari zisizotarajiwa kwa biashara ya kimataifa na usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako