• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM aitaja COVID-19 kama msukosuko mkubwa zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia

    (GMT+08:00) 2020-04-01 10:03:44

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema mlipuko wa COVID-19 ni msukosuko mkubwa zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia kwa sababu ni tishio kwa kila mtu.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iitwayo "Jukumu la pamoja, mshikamano wa dunia: Mwitikio wa athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19", Bw. Guterres amesema msukosuko wa COVID-19 unahitaji mwitikio wa pamoja na wenye ufanisi unaopatikana tu kupitia mshikamano wa dunia nzima, ambao unahitaji watu wote wachangie juhudi, waachane na michezo ya kisiasa na kuelewa kuwa janga hili ni tishio kwa binadamu wote.

    Bw. Guterres ameongeza kuwa tunaelekea taratibu kwenye mwelekeo sahihi, lakini tunahitaji kuharakisha na kufanya juhudi zaidi ili kuweza kushinda vita dhidi ya virusi vya Corona, kuwasaidia watu wenye mahitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako