• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la FAO lahimiza kuzuia mgogoro wa chakula unaosababishwa na maambukizi

    (GMT+08:00) 2020-04-01 11:31:31

    Mkurugenzi mkuu mtendaji wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa Bw. Qu Dongyu hivi karibuni ametoa makala ikiihimiza dunia nzima kuchukua hatua mara moja, ili kupunguza kadri iwezekanavyo athari zinazoletwa na maambukizi ya virusi vya Corona kwa mnyororo wa utoaji wa chakula na kuzuia msukosuko wa chakula unaoweza kutokana na msukosuko huo wa afya ambao utaweza kusababisha kusimama kwa utoaji wa chakula na kupanda kwa bei za chakula.

    Makala hiyo inayoitwa "Tusiyafanye maambukizi ya virusi vya Corona yawe mchezo wa njaa" imesema, hadi sasa maambukizi hayo bado hayajatishia usalama wa chakula. Hakuna haja kuogopa, kwa sababu utoaji wa chakula duniani unaweza kukidhi mahitaji ya kila mtu. Lakini wakati huohuo, tunatakiwa kukabiliana moja kwa moja na changmoto kwamba sehemu zinazokumbwa na ukosefu wa chakula zinaweza kujitokeza na kukatika kwa utoaji wa chakula.

    Makala hiyo pia imesema, mlipuko wa ugonjwa huo na hatua za vizuizi na karanti zinazochukuliwa kwa lengo la kuzuia maambukizi, vimezuia usafirishaji na ugavi wa vitu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako