• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mayanja ageuziwa kibao KMC akipanga kuiburuza FIFA

    (GMT+08:00) 2020-04-01 16:30:54

    Kocha Jackson Mayanga aliyepanga kuishtaki klabu ya KMC kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) akidai kutolipwa madai yake baada ya mkataba wake kuvunjwa, ameambiwa hadai chochote klabuni hapo. Mayanja ambaye mkataba wake ulivunjwa Novemba mwaka jana, kwa sasa ni kocha wa timu ya Kyetume inashiriki Ligi Kuu Uganda. Kocha huyo amesema, licha ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Shirikisho la Soka Tanzanua (TFF) kuiamuru KMC kumlipa fedha hizo, haoni dalili za uamuzi huo kutekelezwa, jambo linalomshawishi kufikisha suala hilo FIFA akiamini kuwa atapatiwa haki yake. Lakini Meya wa Manispaa ya Kinondoni ambaye ni mlezi wa KMC, Benjamin Sitta amesema walishamalizana na Kocha huyo, na kama ana madai yoyote, afuate taratibu na si kulalama katika vyombo vya habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako