• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asema virusi vya Corona ni changamoto kubwa zaidi tangu Umoja huo uanzishwe

    (GMT+08:00) 2020-04-01 18:14:46

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ametoa ripoti kuhusu kukabiliana na athari mbaya za kijamii na kiuchumi zinazosababishwa na virusi vya Corana, na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua kwa pamoja ili kupunguza athari hizo.

    Guterres amesema virusi vya Corona ni changamoto kubwa zaidi tangu Umoja wa Mataifa uanzishwe, hali ambayo inahitaji nchi kubwa za kiuchumi duniani zishirikiane na kuchukua hatua zenye uvumbuzi haraka iwezekanavyo, pia zinapaswa kuzipatia nchi zinazoweza kuathiriwa kirahisi na virusi msaada wa kifedha na kiteknolojia.

    Ameongeza kuwa, nchi zote duniani zinapaswa kuchukua hatua za kiafya kwa pamoja ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, na kutoa umuhimu mkubwa kwa nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi zinazoendelea katika kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na changamoto hiyo. Mbali na hayo, nchi zote zinapaswa kukabiliana na athari mbaya ya kijamii na kiuchumi, na kutilia maanani katika kusaidia watu na mashirika yanayoathiriwa vibaya zaidi na virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako