• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani asema wiki mbili zifuatazo zitakuwa kipindi kigumu kwa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-04-01 18:15:09

    Rais Donald Trump wa Marekani jana amesema nchi hiyo inakumbwa na changomoto kubwa zaidi kihistoria, na wiki mbili zijazo zitakuwa kipindi kigumu zaidi kwa nchi yake, na kusisitiza kuwa kufuata pendekezo la kujikinga na virusi vya Corona kunahusiana na uhai wa watu.

    Mtaratibu wa Ikulu ya Marekani anayeshughulikia mambo ya kupambana na virusi vya Corona Bibi Deborah Birx amewaambia wanahabari kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya hali ya virusi vya Corona nchini humo. Makadirio yaliyotolewa naye yanaonyesha kuwa idadi ya vifo vya watu kutokana na virusi hivyo inaweza kufikia laki 1 hadi 2.4 chini ya hatua za udhibiti, na idadi hiyo ingefikia milioni 1.5 hadi milioni 2.2 bila ya kuchukua hatua hizo.

    Ripoti iliyotolewa na Chuo cha udaktari katika Chuo Kikuu cha Washington imetabiri kuwa, hali mbaya zaidi ya kuenea kwa virusi vya Corona itatokea katika mwezi huu nchini humo, na itaendelea hadi mwezi Juni, na huenda ikatokea tena katika majira ya mpukutiko na majira ya baridi mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako