• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya kuagiza magunia milioni 4 ya mahindi

    (GMT+08:00) 2020-04-01 18:55:55
    Serikali ya Kenya imeidhinisha uagizaji wa magunia milioni 4 ya mahindi ili kuepusha mzozo wa chakula wakati serikali inapambana na kuenea kwa virusi vya corona.

    Mvua kubwa katika miezi nane iliyopita ilisababisha mafuriko, na kuharibu mazao nchini humo.

    Ripoti kuhusu kujitosheleza na chakula iliyotolewa mwezi uliopita na Mtandao wa Mfumo wa Onyo la Mapema iulionyesha kuwa angalau kaunti 17 zitakubwa na upungufu wa chakula kati ya mwezi Februari na Mei.

    Waziri wa Kilimo Peter Munya alisema serikali itanunua magunia milioni mbili ya mahindi meupe kwa matumizi ya binadamu na magunia mengine milioni mbili ya mahindi ya manjano kusindika kama lishe ya wanyama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako