• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 20 wauawa kwa shoti ya umeme nchini Jamhuri ya Kongo

    (GMT+08:00) 2020-04-01 21:03:35

    Watu 20 wameuawa kwa kupigwa na shoti ya umeme baada ya nyaya zenye nguvu kubwa ya umeme kuanguka kutokana na radi pembezoni mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Brazzaville mapema leo.

    Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mjini Brazzaville saa kumi na moja alfajiri ya leo, huenda radi ilikata waya wenye umeme mkubwa unaotoka kwenye gridi ya taifa.

    Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, baadhi ya watu walifariki majumbani mwao na wengine barabarani, na majeruhi wamepelekwa hospitali kupatiwa matibabu.

    Huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako