• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Neymar yupo kwenye hesabu za kurudishwa ndani ya Barcelona, Kane awindwa na Juventus

    (GMT+08:00) 2020-04-02 08:44:40

    Neymar da Silva Santos JĂșnior nyota wa PSG inayoshiriki Ligue 1 yupo kwenye hesabu za kurudishwa ndani ya Barcelona. Akiwa ndani ya PSG ametupia mabao 13 na timu yake inaongoza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 68. Imecheza mechi 27 na kufunga jumla ya mabao 75 msimu huu wa 2019/20. Nyota huyo ana miaka 28 amecheza mechi 15 na ametoa pasi sita za mabao. Naye Harry Edward Kane nyota wa Spurs anasumbuliwa na msuli wa nyama za paja jambo lililomuweka nje ya Uwanja kwa muda mrefu. Inaelezwa kuwa Kane anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho huku Juventus ikitajwa kuiwinda saini yake. Nyota huyo amecheza mechi 20 na amefunga mabao 11 kwenye Ligi Kuu England.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako