• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawaonya wakimbizi waache kutembea nje ya kambi ili kuepuka tishio la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-02 09:03:00

    Mamlaka ya mkoa wa Kigoma nchini Tanzania imewaonya wakimbizi walioko kwenye kambi za mkoa huo waache kutembea nje ya kambi zao, ikiwa hatua ya kujikinga dhidi ya nimonia ya COVID-19.

    Mkuu wa mkoa wa Kigoma Bw. Emmanuel Maganga ametoa onyo kuwa wakimbizi wanaotembea nje ya kambi zao watapoteza hadhi zao za ukimbizi na kufikishwa mahakamani.

    Kwenye mkutano uliojadili njia bora za kulinda mkoa huo dhidi ya tishio la COVID-19, Bw. Maganga amesema, kwa kuwa mkoa wa Kigoma una idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi jirani, kuwaruhusu watembee nje ya kambi zao kutatatiza hatua zinazolenga kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako