• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wahimiza mwitikio wa COVID-19 wakati uchumi wa dunia unakadiriwa kudidimia

    (GMT+08:00) 2020-04-02 10:04:02

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kuzisaidia nchi mbalimbali kukabiliana na mlipuko wa COVID-19, wakati Idara ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja huo DESA imetoa onyo kali kuwa uchumi wa dunia unaweza kupungua kwa asilimia 1 mwaka huu.

    DESA imesema kwenye ripoti yake kuwa hatua za karantini zilizochukuliwa na nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini zimeathiri vibaya sekta za huduma, hoteli na uchukuzi, ambazo kwa ujumla zinatoa zaidi ya asilimia 25 ya nafasi zote za ajira katika nchi hizo.

    Ripoti hiyo imesema athari za hatua hizo zitaenea haraka hadi kwenye nchi zinazoendelea, na pia zinaweza kusababisha kupungua kidhahiri kwa sekta ya uzaliushaji viwandani na kuvuruga minyororo ya ugavi duniani.

    DESA imesema wakati mlipuko wa COVID-19 unakithiri, wasiwasi wa kiuchumi na kukosekana kwa usawa vitaongezeka hata katika nchi zenye mapato ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako