• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona yazidi laki 8.20 kote duniani

    (GMT+08:00) 2020-04-02 10:40:40

    Takwimu kutoka Shirika la Afya la Dunia WHO imeonyesha kuwa hadi mpaka jana, idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona kote duniani imefikia 827,419, na 40,777 kati yao wamefariki. Hadi sasa nchi na sehemu 205 duniani zimekumbwa na maambukizi ya vurisi hivyo, na maambukizi laki 7.40 yako nje ya China.

    Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani zinaonyesha kuwa hadi kufikia jana maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo yamefikia 213,372, na watu 4,757 kati yao wamefariki.

    Kwa upande wa Italia hadi jana watu 110,574 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo, na 13,155 kati yao wamekufa. Wakati huohuo, idadi ya maambukizi nchini Ufaransa imeongezeka hadi 56,989, na 4,032 kati yao wamefariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako