• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bocco atuliza mzuka Simba

    (GMT+08:00) 2020-04-02 16:41:34

    Zikiwa zimesalia wiki mbili kufahamu hatma ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imesimama ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona, nahodha wa Simba John Bocco amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuahidi kikosi chao kitatekeleza kwa vitendo ahadi ya kutetea taji wanaloshikilia. Bocco amesema wachezaji wote wanaendelea na mazoezi binafsi, kwa kuwa wanaamini Ligi itakaporejea, kutakuwa na ushindani zaidi. amesema ushindani utaongezeka kutokana na idadi ya michezo iliyobaki kuwa michache na kila timu ikihitaji kuvuna pointi na kutimiza malengo. Simba inaongoza Ligi hiyo ikiwa na pointi 71, na imebakiza mechi 10 na inahitaji point 14 tu kufikisha 85 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine msimu huu, na hivyo kuendelea kutetea ubingwa wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako