• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rachier ataka kufuatwa kwa utawala wa sheria katika uchaguzi wa FKF

    (GMT+08:00) 2020-04-02 16:41:50

    Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu nchini Kenya Ambroce Rachier amewataka viongozi wa soka kuwa na mapenzi ya dhati na mchezo huo kwa kuwa siasa nyingi zinaharibu taswira ya soka nchini humo. Rachier, ambaye pia ni mwenyekiti wa timu ya Gor Mahia, ametoa wito wa kufuatwa kwa utawala wa sheria wakati uchaguzi unapofanyika. Uchaguzi katika Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) umefutwa mara mbili na Mahakama ya Usuluhishi wa masuala ya Michezo. Mahakama hiyo imelitaka Shirikisho hilo kuunda kamati huru itakayosimamia uchaguzi huo. Rachier amesema, vurugu hizo hazileti picha nzuri ya mchezo wa soka nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako