• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa waahirishwa mpaka mwakani kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-02 17:41:11

    Uingereza imesema itaahirisha mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (COP26) uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu hadi mwakani kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Taarifa iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imesema, tarehe mpya ya kufanyika mkutano huo mwaka ujao huko Glasgow chini ya mwenyeji Uingereza kwa kushirikiana na Italia zitatajwa baadaye baada ya majadiliano ya pande husika.

    Taarifa hiyo imesema, uamuzi huo umechukuliwa na wawakilishi wa Tume ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa pamoja na wajumbe kutoka Uingereza na Italia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako