• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani yafikia laki 8.2

    (GMT+08:00) 2020-04-02 17:52:03

    Takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO zinaonyesha kuwa, mpaka jana saa 12 jioni kwa saa za Ulaya ya kati, idadi ya jumla ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani ilifikia 827,419 na watu 40,777 wamefariki kutokana na virusi hivyo.

    Mpaka sasa, nchi na sehemu 205 duniani zimethibitisha kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, na watu zaidi laki 7.4 nje ya China wameambukizwa virusi hivyo.

    Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha The Johns Hopkins zinaonyesha kuwa, mpaka saa 1 usiku jana, Marekani ilikuwa na kesi 213,372 za virusi hivyo, na watu 4,757 wamefariki.

    Nchini Italia, idadi ya kesi za virusi hivyo imefikia 110,574 na kusababisha vifo 13,155.

    Wizara ya afya ya Ufaransa jana imetangaza kuwa, nchi hiyo ina kesi 56,989 za virusi vya Corona ambayo iliongezeka kwa 4,861, na watu waliofariki kutokana na virusi hivyo ni 4,032.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako