• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika yaendelea kuongezeka

    (GMT+08:00) 2020-04-02 17:52:29

    Takwimu zilizotolewa jana Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika zinaonesha kuwa, idadi ya jumla ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imefikia 6,213. Ili kukabiliana na maambukizi hayo, nchi mbalimbali zilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuongezeka nguvu ya upimaji.

    Tume ya uchaguzi nchini Ethiopia imetangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu, ikiwa ni juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vya Corona.

    Wizara ya afya nchini Afrika Kusini jana ilisema, kupima watu wengi ni njia muhimu ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo, na ilikadiria kuwa itaongeza uwezo wa upimaji na kupima watu 30,000 kila siku.

    Idadi ya kesi za virusi vya Corona nchini Kenya jana iliongezeka kwa 22, ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi kwa siku moja.

    Nchini Uganda, serikali ya nchi hiyo imetangaza kuwa itaanza kugawa chakula kwa watu maskini zaidi milioni 1.5 waliozuiliwa majumbani kutokana na maambukzi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako