• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Wuhan kurejesha utaratibu wa maisha ya kawaida

    (GMT+08:00) 2020-04-02 17:53:07

    Mkurugenzi wa Kamati ya Afya ya China Bw. Ma Xiaowei amesema, mlipuko wa virusi vya Corona nchini China kwa sasa unakaribia kudhibitiwa kikamilifu, na mji wa Wuhan ulioathirika zaidi na mlipuko huo, unaanza kurejea kwenye utaratibu wa kawaida.

    Bw. Ma amesema, kuanzia tarehe 8, mwezi huu, mji wa Wuhan utaondoa vizuizi vya usafiri katika mji huo na kurejesha safari zote za ndege za ndani. Hivi sasa, mji wa Wuhan unajiandaa kuanza tena uzalishaji na kufungua masoko ili kupunguza hasara kutokana na mlipuko wa virusi hivyo.

    Takwimu zilizotolewa na Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya mkoa wa Hubei zinaonesha kuwa, mpaka mwishoni mwa mwezi uliopita, kiwango cha kuanza upya uzalishaji katika mji wa Wuhan kimefikia asilimia 85.4, na kwa mkoa wa Hubei kimefikia asilimia 93.8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako