• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yapinga malalamiko dhidi ya China kwa kutoa takwimu zisizo za kweli

    (GMT+08:00) 2020-04-02 17:53:30

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limepinga malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari dhidi ya China kuhusu nchi hiyo kutoa takwimu zisizo za kweli.

    Mkurugenzi wa WHO anayeshughulikia miradi ya dharura ya afya Dr. Michael Ryan amesema, takwimu zilizotolewa na nchi mbalimbali zina uthibitisho mkubwa wa kisayansi. Pia amesema, si vizuri kuilaumu nchi fulani kwa kutoa takwimu zisizo za wazi, na kuongeza kuwa WHO itashirikiana na kila nchi kupata takwimu sahihi zaidi. Hivi sasa, WHO imepata ripoti 7 za uchunguzi wa kuenea kwa virusi vya Corona, miongoni mwao, 4 zinatoka China.

    Aidha mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus pia amesema, virusi vya Corona ni virusi vipya kwa binadamu, hivyo ni lazima kuaminiana na kutekeleza vizuri kazi ya kuthibitisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako