• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza jamii ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-02 18:08:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, China inaitaka jamii ya kimataifa kuitikia wito wa Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono mashirika ya kimataifa ikiwemo Umoja huo na Shirika la Afya Duniani WHO kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Hivi karibuni, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema, virusi hivyo ni changamoto kubwa zaidi inayomkabili binadamu tangu kuanzishwa kwa Umoja huo. Ameongeza kuwa, nchi kubwa za kiuchumi duniani zinatakiwa kuchukua hatua madhubuti, na kutoa misaada kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo kadiri ziwezavyo.

    Hua amesema, kutokana kukabiliwa na changamoto hiyo kubwa, jamii ya kimataifa inapaswa kushikamana na kushirikiana ili kuishinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako