• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya ndege duniani huenda yakaingia hasara ya $61bn , yasema IATA

    (GMT+08:00) 2020-04-02 20:39:56

    Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) kimetabiri kuwa mashirika ya ndege duniani huenda yakatumia $61 bilioni ya fedha zao za akiba katika nusu ya pili ya mwaka huu,huku maambukizi ya virusi vya corona yakizidi kuenea.

    IATA imeonya kuwa mashirika ya ndege huenda yakaishiwa na pesa kufikia mwisho wa mwezi Juni,na hii huenda ikasababisha hasara za zaidi ya $39 bilioni.

    Mapato yanatarajiwa kupungua kwa asilimia 68 katika kipindi hicho.

    IATA ambayo inawakilisha mashirika ya ndege 290 yanayojumlisha asilimia 82 ya usafiri wa anga,imetoa wito kwa serikali za mashirika hayo kuingilia kati.

    Mkurugnezi Mkuu wa IATA , Alexandre de Juniac, alisema mashirika ya ndege hayawezi kupunguza gharama na kumudu athari za janga za corona bila msaada kutoka kwa mataifa yao.

    Juniac alisema athari ya utumizi wa pesa itakuja kuongezwa zaidi na malipo ya fedha za tiketi zinazokadiriwa kuwa $35bn ambazo wateja walinunua na hatimaye safari kufutwa kutokana na vikwazo vya usafiri vilivyotolewa na mataifa mengi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako