Miongoni mwa sababu walizozieleza ni watalii kusitisha safari zao za kuja kutalii na kupanda Mlima Kilimanjaro.
Akizungumza na wanahabari jana ,Meneja wa TRA, Mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi, alisema kuwa licha ya maombi ya wafanyabiashara hao, TRA imekusanya zadi ya Sh. bilioni 10 sawa na asilimia 85 ya makisio yake kwa mwezi Machi mwaka huu.
Alisema TRA kila siku kuanzia mwezi Januari mwaka huu imekuwa ikipokea wastani wa barua za maombi zaidi ya 30 kila siku kutoka kwa wafanyabiashara wakiomba kusimamisha biashara zao kwa muda, wengine moja kwa moja kutokana na mwenendo wa biashara zao.
Aidha alisema tishio la maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa homa ya mapafu corona, limechangia kwa kiasi kikubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |