Haya ni kwa mujibu wa Ripoti mpya ya kazi iliyotolewa na Shirika la Kitaifa la Takwimu nchini Kenya (KNBS).
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa wakenya wengine 600,000 walilazimika kufanya kazi za kiwango cha chini zenye mshahara mdogo baada ya kutokuwa na kazi kwa muda mrefu.
Kwa jumla,kati ya mwezi Oktoba na Disemba mwaka jana,kulikuwa na wakenya 929,595 ambao hawakuwa wameajiriwa,ikimaanisha kuwa hawakuwa na kazi lakini wamekuwa wakitafuta katika kipindi cha wiki nne kabla ya utafiti huo kufanywa.
Kulingana na Ripoti hiyo,kiwango cha kitaifa cha ukosefu wa ajira kilikuwa asilimia 4.9 katika robo ya nne ya mwaka jana ikilinganishwa na asilimia 5.3 katika robo ya tatu ya mwaka huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |