• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaweza kupata mavuno makubwa ya nafaka licha ya mlipuko wa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-02 20:41:28

    Wizara ya Biashara ya China leo imesema, kuna uwezekano mkubwa kuwa China itashuhudia mavuno makunwa ya nafaka kwa mwaka huu kwa kuwa hifadhi ya kutosha na uzalishaji mzuri wa kilimo umehakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha licha ya mlipuko wa virusi vya Corona.

    Ofisa kutoka Wizara hiyo Wang Bin amesema, China imeshuhudia mavuno mazuri kwa miaka kadhaa, kwa ukusanyaji na hifadhi kubwa, na bei ya nafaka kuendelea kuwa ya utulivu. Amesema China, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa chakula duniani, mavuno ya nafaka yamefikia tani milioni 664 mwaka jana, ukiwa ni mwaka wa 16 mfululizo.

    Amesema nafaka zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje ni kavu kama vile soya, huku mchele na ngazo zinazoagizwa kutoka nje zikichukua asilimia moja na mbili ya matumizi ya jumla ya ndani ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako