• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama mbalimbali duniani vyatoa wito wa kuimarisha ushirikiano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-02 20:41:54

    Chama cha Kikomunisti cha China pamoja na vyama vingine zaidi ya 230 vya kisiasa kutoka zaidi ya nchi 100 duniani vimetoa wito wa pamoja, wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Wito huo unasema virusi vya Corona ni tishio kubwa na la ghafla zaidi dhidi ya afya ya binadamu na maendeleo na amani duniani, hivyo nchi zote zinapaswa kuchukulia usalama na afya ya wananchi wake katika nafasi ya kwanza. Pia zinapaswa kuchukua hatua zenye nguvu za kuzuia kuenea kwa virusi, kufuata mawazo ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kusaidiana na kuungana mkono, na kukusanya rasilimali na nguvu zote, ili kushinda vita dhidi ya virusi hivyo ambavyo ni adui wa pamoja wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako