• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BIFU: Tambo na Majigambo kati ya Benzema na Giroud mtandaoni

    (GMT+08:00) 2020-04-03 08:34:57

    Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Chelsea ya England Olivier Giroud mwenye miaka 33, amejibu kejeli za mfaransa mwenzake anayekipiga Real Madrid Karim Benzema kwa kumringishia mafanikio yake. Akiulizwa maswali kupitia Instagram, Benzema mwenye miaka 32, ambaye alikuwa akilinganishwa uwezo wake na Olivier Giroud nani mkali akatoa jibu ambalo wengi walitafsiri kama dharau kwa Giroud. Benzema alisema yeye ni sawa na gari la Formula 1 na kumwita Giroud ni kama Go Kart yaani magari ya kuchezea watoto. Baadae Befoot walimtafuta Giroud na kumuuliza kuhusiana na maoni ya Benzema juu yake na kujitamba yeye ni Bingwa wa Dunia kwa kuwa kachukua World Cup 2018 wakati Benzema akiwa hajawahi. Benzema aliachwa kuitwa timu ya taifa ya Ufaransa iliyokuwa inafundishwa na kocha Didier Deschamps toka 2015 kutokana na kuwa katika uchunguzi wa kudaiwa kujihusisha na kurekodi tape ya ngono. 2018 kuelekea fainali za Kombe la Dunia wengi walitarajia kuwa Benzema anaweza kuitwa lakini aliachwa na kuitwa Olivier Giroud kitu ambacho kilizua mjadala mzito mtandaoni, Ufaransa ikiwa na Giroud ilishinda Kombe la Dunia licha ya Giroud kumaliza michuano hiyo bila goli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako