• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Willian awekwa kwenye rada za Juventus na Tottenham, huku Lovren huenda akaondoka Liverpool msimu ujao

    (GMT+08:00) 2020-04-03 08:35:41

    Willian nyota anayekipiga ndani ya Chelsea amewekwa kwenye rada za Juventus na Tottenham ambazo zimetajwa kumuwinda kiungo huyo. Willian alikuwa akihusishwa kutimka ndani ya Klabu ya Chelsea katika usajili uliopita lakini sasa Juventus wanaonekana kushikilia bango la kutaka kumsajili. Imeelezwa kuwa nyota huyo anataka kusalia ndani ya London hivyo huenda Spurs wakaipata saini yake. Kiungo huyo mpaka sasa hana uhakika wa kubaki ndani ya Chelsea baada ya kuambiwa aongeze mkataba wa mwaka mmoja huku yeye hesabu zake zikiwa ni kusaini mkataba wa miaka miwili. Naye beki anayekipiga ndani ya Liverpool Dejan Lovren mwenye miaka 30 huenda akaondoka msimu ujao. Beki huyo amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza kilicho chini ya Jurgen Klopp. Inatajwa kuwa Arsenal, Spurs na West Ham zipo kwenye hesabu ya kuwania saini yake. Timu yake ikiwa imecheza mechi 29 amecheza mechi tisa pekee za Ligi Kuu England na ametoa pasi moja ya bao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako