Saudi Arabia imetoa mwito kwa jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta OPEC na nchi zinazozalisha mafuta zisizo za OPEC zinazoongozwa na Russia kufanya mkutano wa dharura, na kutarajia kufikia makubaliano ya haki ili kutuliza soko la mafuta. Makundi hayo mawili yalishindwa kufikia makubaliano mwanzoni mwa mwezi Machi kuhusu kupunguza uzalishaji mafuta, baada ya hapo Saudi Arabia ilitangaza kuongeza uzalishaji na kushusha bei ya mafuta. Katika mwezi uliopita, bei ya mafuta ilishuka kwa kiasia kikubwa katika soko la kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |