• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 duniani yazidi milioni moja

    (GMT+08:00) 2020-04-03 09:14:14

    Takwimu zilizotolewa jana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani zimeonesha kuwa, idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona waliothibitishwa dunia kote imeongezeka na kuwa zaidi milioni moja.

    Takwimu zimeonesha kuwa hadi kufikia jana, saa 5 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, idadi ya wagonjwa watu wenye virusi vya Corona duniani imefikia 1,002,159, na idadi ya vifo imefikia 51,485.

    Takwimu hizo pia zimeonesha kuwa, Marekani imekuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wagonjwa waliothibitika, ambapo idadi ya watu wenye virusi hivyo imefikia 236,339.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako