• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya yafikia 110

    (GMT+08:00) 2020-04-03 10:03:21

    Serikali ya Kenya imesema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo imefikia 110, na serikali itachukua hatua thabiti kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

    Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe amesema katika siku iliyopita, jana watu 29 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, wakiwemo wananchi 28 wa Kenya na raia mmoja wa Congo. Amesema serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti kupambana na virusi hivyo, na kuwahimiza watu wote wafuate kanuni za kujikinga dhidi ya virusi.

    Ameongeza kuwa wagonjwa wawili waliokuwa Nairobi na Mombasa wamefariki, na kuifanya idadi ya vifo kutokana na virusi hivyo nchini Kenya ifikie watatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako