• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump aagiza kuharakisha uzalishaji wa mashine za kupumulia

    (GMT+08:00) 2020-04-03 10:04:00

    Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena ameagiza kuharakisha uzalishaji wa mashine za kupumulia ambazo zinawasaidia sana wagonjwa wenye hali mbaya wa COVID19, ili kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona nchini Marekani.

    Taarifa inasema rais Trump amewaagiza mawaziri wa afya na usalama wa ndani wasaidie kuondoa vizuizi vyote na kuhakikisha kampuni 6 za Marekani zinapata vifaa vinavyohitajika katika uzalishaji wa mashine za kupumulia.

    Majimbo nchini Marekani yamejiunga kwenye ushindani wa kununua mashine hizo, kutokana na kwamba akiba ya vifaa hivyo muhimu inakaribia kwisha. Tarehe 27 Machi, rais Trump aliwahi kuiagiza kampuni ya GM ya kuteneneza magari izalishe mashine za kupumulia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako