• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa Angola nchini China wachangia kukabiliana na corona nyumbani

    (GMT+08:00) 2020-04-03 10:25:18

    Video kuhusu uzoefu na mbinu za kujikinga na virusi vya corona iliyotengenezwa na wanafunzi wa Angola wanaosoma mjini Xiamen, China imejulikana kwenye mtandao.

    Rais wa Angola João Manuel Gonçalves Lourenço wa Angola amewapongeza wanafunzi hao na kutoa wito wananchi wote wajifunze. Waziri wa nchi hiyo anayeshughulikia uratibu wa kazi ya kukabiliana na ugonjwa huo alisema, uzoefu uliopatikana nchini China unasaidia sana katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kote duniani, nchi yake na China zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika juhudi za kuzuia k uenea kzi wa virusi hivyo.

    Nchini Ghana, serikali ilitangaza amri ya kutotoka nje ya wiki mbili katika mkoa wa Greater Accra na mji wa Kumasi, amri hiyo imeanza kutekelezwa Machi 30. Kampuni za China nchini Ghana zilichangia vifaa vinne vya kufanya mkutano kwa njia ya video, ambavyo vinafungwa katika wizara ya afya na hospitali. Vifaa hivyo vinasaidia kuongeza ufanisi wa mawasiliano na kupunguza hatari ya kuambukizwa inayoweza kuletwa kutokana na watu kukutana ana kwa anauso kwa uso.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako