• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo duni la Dharavi la India latokea kesi ya kwanza ya maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-03 10:47:57

    Mwanamume wa India mwenye umri wa miaka 56 aliyeishi katika eneo duni la Dharavi mjini Mumbai alithibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona tarehe mosi mwezi huu, na kufariki njiani kabla ya kufikishwa hospitali. Familia yake imewekwa kwenye karantini kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya, na jengo la makazi yake pia limefungwa.

    Mumbai ni mji mwenye watu wengi zaidi nchini India, na eneo duni la Dharavi lenye kilomita 2 tu za mraba ni eneo moja lenye watu wengi zaidi kwenye mji huo, ambalo lina watu laki 7 hadi milioni 1, ni moja ya maeneo duni makubwa zaidi barani Asia.

    Kutokea kwa mtu wa kwanza mwenye maambukizi ya virusi vya Corona kwenye eneo duni la Dharavi kumewaletea watu wa huko wasiwasi mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako