• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Champions League, Europa League bado hali tete

    (GMT+08:00) 2020-04-03 17:16:13

    Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza maamuzi magumu kuhusiana na michuano ya ligi ya mabingwa barani humo (UEFA Champions League) na Kombe la Shirikisho (UEFA Europa League) wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona. UEFA wametangaza kuahirisha michuano hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona kuendelea kushika kasi barani Ulaya na kwingineko duniani. Licha ya michuano hiyo kuwa imesimamishwa kwa muda usiojulikana, lakini inaripotiwa inaweza kuendelea Julai au Agosti 2020, hii pia ni kupisha Ligi za ndani ziweze kumalizika na kuangalia mwelekeo wa maambukizi ya Corona kama yatakuwa yamepungua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako