• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RUGBY: Amonde afikiria hatua mpya baada ya michezo ya Olimpiki kuahirishwa

    (GMT+08:00) 2020-04-03 17:17:33

    Nahodha wa timu ya Rugby ya Kenya Sevens Andrew Amonde yuko njia panda katika kazi yake kimataifa naada ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo kuahirishwa mpaka mwakani. Amonde alikuwa amepanga kustaafu mchezo huo baada ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo ambayo awali ilipangwa kufanyika Julai hadi Agosti mwaka huu. Amesema hivi sasa anasubiri kuangalia mambo yatakavyokwenda na kushauriana na watu wake wa karibu kuhusu hatua inayofuata. Amonde na timu yake ya Kenya Sevens walijiweka karantini kwa siku 14 zilizomalizika jumatano baada ya kurejea nchini humo kutoka kwenye mashindano ya Dunia ya Rugby Sevens Las Vegas na Vancouver.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako