• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha wa Simba akabidhi faili la usajili

    (GMT+08:00) 2020-04-03 17:17:49

    Wakati ligi ikiwa imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amekabidhi faili la usajili wa msimu ujao kwa mabosi wake huku jina la kiungo wa Yanga, Mkongomani Papy Tshishimbi likikosekana. Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema, kwenye kipindi hiki tayari kocha huyo ameshawapa majina ya wachezaji ambao anawataka katika kikosi hicho kwa msimu ujao, huku pia akiainisha nani waachwe huku wakiweka bayana kwamba hawatamkosa mchezaji yeyote katika orodha hiyo. Amesema tayari wanayo majina ya wachezaji ambao watakuwepo kwenye kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kocha huyo kuwapa faili zima la nani anamuhitaji kwenye kikosi chake na nani hamtaki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako