• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wadogo wadogo Kenya wafurahia kufunguliwa kwa soko baada ya kufungwa kutokana na corona

    (GMT+08:00) 2020-04-03 18:27:11

    Wachuuzi wa kuuza vyakula katika Soko kuu katika eneo la Thika nchini Kenya wamepata afueni baada ya Soko hilo kufunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda wa wiki moja.

    Wiki iliyopita masoko kadha katika kaunti ya Kiambu yalifungwa ili kukabiliana na homa kali ya Covid-19.

    Baadhi ya masoko yaliyofungwa katika kaunti hiyo ni ya Madaraka, Ruiru, na Githurai. Hatua hiyo ilichukuliwa ili kunyunyizia dawa ya vieuzi (Sanitizer) katika masoko hayo na kuhamasisha wachuuzi hao jinsi ya kujikinga na homa hiyo bila kujumuika kwa pamoja.

    Awali gavana wa kaunti hiyo Dkt James Nyoro alisema kila Soko litapulizwa dawa kabla ya kuruhusiwa kurejelea shughuli zake. Alisema masoko ya Githurai na Ruiru yangefunguliwa baada ya kunyunyiziwa dawa.

    Hata hivyo wachuuzi wa kuuza nguo za mitumba na viatu wameonywa kutoingia katika Soko hiyo kwa sababu vyakula havistahili kuwa mahali pamoja na nguo. Mji wa Thika unaendelea kuwa na watu wachache baada ya bishara nyingi kufungwa. Biashara zinazoendelea kidogo ni matatu , bodaboda, na maduka machache ya kuuza nguo na simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako