• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wataka kupunguziwa mzigo wa kodi

    (GMT+08:00) 2020-04-03 18:28:03
    Wafanyabiashara wanaolipa kodi ya jumla kwa mwaka nchini Kenya wameitaka mamlaka ya kodi nchini humo kuwapunguzia mzigo wa kodi wakati huu ambapo Kenya inapambana na janga la maambukizi ya virusi vya Corona. Wafanya biashara hao wamesema hivi sasa wanakumbwa na changamoto kubwa ya kibiashara na endapo Mamlaka hiyo haitawapunguzia mzigo huo wa kodi basi hunda wakashindwa kuokoa biashara zao. Miongoni mwa wafanya biashara hao ni wale ambao hulipa kodi kwa mwaka. Wafanya biashara hao huwa wanatakiwa kulipa kodu na haijalishi kama wametengeneza faida au hasara. Kilio hicho kinakuja wakati ambapo tayari rais Uhuru Kenyatta amepunguza kodi kwa mapato ya wafanya kazi na wakati huo huo kulitaka bunge la Kenya kupunguza kodi kwa ajili ya kuwasaidia wafanya biashara wadogo wadogo. Biashara nyingi hivi sasa zimefungwa huku nyingine zikijikokota kutokana na marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi kutokana na virusi vya Corona. Wadadisi wa mambo ya uchumi wanaona hali ya kiuchumi kwa wakenya huenda ikawa ngumu zaidi kama maambukizi ya virusi vya Corona yataendelea.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako