• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa ngano walalamikia kupunjwa na walanguzi

    (GMT+08:00) 2020-04-03 18:28:21
    Wakulima wa ngano katika mkoa wa Mbeya nchini Tanzania wameiomba Serikali kutoa bei elekezi ya zao hilo ili kuwanusuru kutoka kwa walanguzi. Wakulima hao wanalalamika kuwa walanguzi hao hununua bidhaa hiyo kwa bei ya chini ikilinganishwa na gharama za uzalishaji. Wakizungumza kwenye uhamasishaji wa kilimo cha zao hilo ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Tari- Uyole, mjini Mbeya, walisema wamekuwa wakilazimishwa kuuza mazao yao kwa bei ya kati ya Sh. 8,000 na 15,000 kwa ndoo ya plastiki yenye ujazo wa lita 20. Wakulima hao wameiomba serikali kutafuta mbinu za kuwasaidia wakulima wasidhulumiwe na walanguzi hao kwa kununua ngano kwa bei ya kutupa, kwani wamekuwa wakitumia nguvu na gharama kubwa katika uzalishaji wa zao hilo na kwamba bei hiyo haiwanufaishi. Kilio hicho kinakuja wakati ambapo serikali imeanzisha mradi wa kuwezesha wakulima katika kilimo cha ngano kwa ufadhili wa Benki ya Afrika baada ya kubaini kuwa kilimo cha zao hilo kina tija katika kuwakwamua wananchi kiuchumi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako